Kocha wa klabu ya Tottenham Antonio Conte amesema hajawahi kua na wasiwasi na ubora wa washambuliqji wake wawili Heung ming Son na Harry Kane kocha huyo amezungumza hayo wakati wakijiandaa na mchezo wao wa wikiendi hii dhidi ya klabu ya Everton.
Heung ming Son ambae alimaliza msimu uliokwisha akiwa kama mfungaji bora lakini ndani ya msimu huu alianza vibaya kabla ya kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao sita dhidi ya klabu ya Leicester City mwezi uliomalizika.
Son ambae alifunga mabao mawili katikati ya wiki katika ligi ya mabingwa ulaya katika ushindi wa mabao matatu kwa mbili dhidi ya Frankfurt ya ujerumani na kuanza kurejesha makali yake msimu huu.
Kutokana na kiwango anachokionesha sasa mchezaji huyo kinamfanya kocha Antonio Conte kuaminia wachezaji hao na kusema kuna kipindi mchezaji anapitia anashindwa kufunga lakini haimaanishi kua sio mchezaji bora.
“Inaweza kutokea wakati unakawa na kipindi ambacho huwezi kufunga au ukawa na bahati mbaya, Lakini narudia, Tunaongelea washambuliaji muhimu. Alisema Antonio Conte wakati anazungumzia washambuliaji wake wawili bora.

