Beki wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza Reece James inaelezwa ana uwezekano wa kuikosa michuano ya kombe la dunia inayotarajiwa kuanza mwezi Novemba nchini Qatar kutokana na majeruhi yaliyompata.
Beki Reece James alipata majeruhi katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya siku ya Jumanne dhidi ya Ac Milan ya nchini Italia katika dimba la San Siro ambapo mchezaji huyo ambaye alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kupata majeraha hayo ya goti na taarifa kutoka huenda akawepo nje kwa kipindi kirefu.
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza kama atakuwepo nje kwa kipindi kirefu kwa majeraha hayo ya goti kama ilivyoelezwa basi ataweza kuikosa michuano ya kombe la dunia ambayo imebakiza siku kadhaa ili kuanza pale nchini Qatar.
Beki huyo kijana kutoka akademi ya Chelsea amekua na kiwango bora sana tangu apandishwe timu ya wakubwa lakini kwa misimu hii miwili amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara.
Reece James anakwenda kufanya klabu yake ya Chelsea kupata wakati mgumu kwenye upande wa kulia wa klabu kwasababu ya uwezo ambao amekua akiuonesha ndani ya timu hiyo na kukiwa hakuna mbadala sahihi wa kuweza kucheza kwa ubora anaouonesha beki huyo.

