Kocha Mkuu wa kikosi cha Kagera Sugar, Mecky Mexime baada ya kupata sare dhidi ya Simba amesema kuwa wao wamepata ushindi.
Mchezo huo ulipigwa jana jumatano kwenye Uwanja wa Kaitaba na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mexime alisema “Kwanza kwa hizi mechi mbili nilizopata sare kwangu mimi nimeshinda kutokana na aina ya timu nilizocheza nazo.
“Nawapongeza vijana wangu kwa kupambana na kufanya kazi nzuri, sisi kwa upande wetu tumeshinda Licha ya kuwa wao wataona wamepoteza kwani Simba wapo kwenye mbio za ubingwa.”

