Klabu ya Tanzania Prisons imefanikiwa kuibuka kidedea dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa derby ya Mbeya uliopigwa jijini Mbeya katika uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine.
Mchezo huu wa ligi kuu ya NBC uliopigwa jijini Mbeya ulikua ukisubiriwa kwa hamu kwani ni mchezo wa mahasimu kutoka jijini humo, Na mchezo huu unatambulika kama derby ya Mbeya kwani mchezo huu unakutanisha mahasimu wa jiji hilo.
Kama ilivyo kawaida mchezo wa mahasimu hua wenye kasi, Nguvu na mahesabu makali ndivyo pia mchezo kati ya Tanzania Prisons na Mbeya City ulivyokua, Maana mchezo ulianza kwa kasi huku nguvu ikitumika na akili nyingi.
Klabu ya Tanzania Prisons ilifanikiwa kupata bao la mapema kupitia kwa Zabona khamis dakika ya 27 ya mchezo, Baada ya kuonesha mchezo mzuri ndani ya dakika hizo na mpaka mapumziko Prisons walikua mbele kwa bao moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi tena huku vilabu vyote vikionekana kutafuta bao zaidi Mbeya City walioonekana kutafuta bao bao la kusawazisha, Lakini Prisons walifanikiwa tena kupata bao la kupitia kwa Samson Mbangula dakika ya 47 ya mchezo.
Klabu ya Mbeya City ilionekana kupambana ipate bao kwa kila namna huku wenzao wakiwa mbele kwa mabao mawili kwa bila, Mpaka pale dakika ya 61 Baraka Mwalubunju alipoipatia bao la kusawazisha na la kufutia machozi klabu ya Mbeya City na kufanya ubao kusomeka mabao mawili kwa moja mpaka mchezo unamalizika.
Klabu ya Tanzania Prisons imefanikiwa kupata alama tatu muhimu dhidi ya mahasimu wao Mbeya City na kuwafanya kufikisha jumla ya alama 21 na kusalia nafasi ya 11 wakizidiwa na mahasimu zao Mbeya City kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa kwani wamelingana alama.

