LICHA ya kuwa wamewekewa milioni 20 mezani ili waifunge Yanga, uongozi wa Tanzania Prisons umefunguka wazi kuwa wanataka kwenda kutonesha kidonda cha Yanga cha kufungwa na Ihefu FC.

 

 

Prisons: Tunakwenda kutonesha kidonda cha Yanga

 

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Tanzania Prisons Jackson Mwafulango ameweka wazi kuwa, wanachohitaji ni kuwafunga Yanga kwa namna yoyote ile ili waweze kuongeza nafasi kwenye msimamo wa ligi.

Mwafulango alisema: “Tutakwenda kuwapa ‘taste’ nyingine ya ugumu Wananchi. Tunakwenda kupiga palepale kwenye kidonda, huo ndiyo mpango wetu, tunakwenda kutonesha kidonda chao.”

Maneno hayo ya Mwafulango yalisindikizwa kwa msisitizo na kauli ya nahodha wa klabu hiyo Benjamin Asukile naye alisema: “Tunakwenda kupiga staili inaitwa mixer kwenye mchezo wetu dhidi ya Yanga. Muhimu kwetu ni alama tatu kwenye mchezo huo.”

Prisons watashuka dimbani kesho kutwa Jumapili kwenye uwanja wa Mkapa saa 1 usiku kusaka alama tatu mbele ya vinara wa ligi Yanga ambao walitoka kupoteza pale kwenye dimba la Highland Estate Mbarali Mbeya dhidi ya Ihefu kwa bao 1-0.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa