Gadiel Afungiwa Mechi Tatu

Beki wa klabu ya Simba Gadiel Michael amefungiwa michezo mitatu na faini ya shilingi laki tano za kitanzania baada ya kuvunja kanuni na taratibu zilizowekwa na bodi ya ligi kuu.

Mchezaji huyo amekumbana na adhabu baada ya kuelezwa alilazimisha kuingia uwanjani masaa sita kabla ya mchezo na kumwaga vitu vyenye asili ya ungaunga na kusababisha bodi ya ligi kutoa adhabu kwa mchezaji huyo.gadielInaelezwa Gadiel alilazimisha kuingia uwanjani kwa madai ya kutaka kukagua uwanja lakini walinzi hawakumruhusu kwakua haukua mda rasmi wa kuingia uwanjani, Lakini mchezaji huyo alitumia hila na kuweza kuingia uwanjani na kwenda moja kwa moja katikati ya uwanja na kumwaga vitu venye ungaunga.

Baada ya mchezo huo nambari 37 kutokea uvunjifu wa kanuni kamati imeamuru mchezaji Gadiel Michael kukosa michezo mitatu na faini ya shilingi Laki tano.gadielHii inakua mara ya pili kwa siku za hivi karibuni mchezaji kufungiwa kutoakana na mambo kama haya, Kwanii wiki moja nyuma rungu lilimuangukia Shafiq Batambuze wa Singida Big Stars  ambae alikutwa na hatia ya kuingia uwananjani kabla ya muda ulioruhusiwa na kufungiwa michezo mitatu na faini juu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.