Timu ya Tanzania Prisons Maarufu kama Wajela jela FC, wameingia makubaliano ya mkataba wa udhamini na kampuni ya usafirishaji wa mizigo kwa njia ya bahari Silent Ocean kwa upande wa chakula, maji, na malazi.

Tanzania Prisons Walamba Mihela

Silent Ocean, wanakuwa ndio wadhamini wakuu wa klabu hiyo kwa mwaka mmoja na mkataba huo una kipengele cha kuongeza kwa miaka ya mbele.

Tanzania Prisons Walamba Mihela

Mwenyekiti wa Tanzania Prisons, Enock Mwanguku alitaja maelezo ya vipengele vya udhamini huo.

“Silent Ocean ni kampuni kubwa ambayo imeidhamini Tanzania Prisons katika maeneo yafuatayo, masuala ya chakula, maji na malazi ambayo ni zaidi ya Milioni 50”

Aidha Mwanguku alitaja sababu zilizowafanya kutaka kushuka daraja msimu uliopita.

“kuna kipindi kuna kupwa na kujaa, huweza kuwa na muendelezo kila mwaka hata timu za Ulaya huwa zinayumba kidogo. Lakini ukiangalia mechi yetu ile ya mwisho ule mpira uliopigwa huwezai kuamini kama hii timu inataka kushuka”

 

Tanzania Prisons Walamba Mihela

Nae Mkuu wa Idara ya Mauzo na Masoko wa Silent Ocean, Mohamed Kamilagwa alisema kuwa wameona sekta ya michezo ina fursa nyingi sana. Na wanayofuraha kuwa sehemu ya Tanzania Prisons ambayo ni taasisi ya Serikali wanaamini ina nidhamu na Ari ya kupambana.

Tanzania Prisons Walamba Mihela

Udhamini huu wa Tanzania Prisons utaisaidia timu hiyo kufanya vizuri kwenye michezo yake, na hii inaifanya Prisons kuungana na Klabu ya KMC ambayo nayo wiki iliyopita, iliingia mkataba na Kampuni ya michezo ya kubashiri Meridianbet Tanzania mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Milioni 300 kama mdhamini mkuu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa