Aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Thomas Tuchel amevunja ukimya kutokana na kile kilichomkuta siku si nyingi baada ya kuachana na klabu yake ambayo aliipenda. Tuchel avunja ukimya huo kwa kusema kuwa;

 

Tuchel 49 Avunja Ukimya

Hii ni moja ya kauli ngumu sana ambayo nimewahi kuandika, na ni moja ambayo nilitarajia nisiingehitaji kufanya kwa miaka mingi. Nimehuzunika sana kwamba muda wangu Chelsea umefika mwisho

Hicho ndicho alichokiandika Thomas Tuchel katika akaunti yake ya Twitter huku ikionekana kuwa ameumia sana kuondoka klabuni hapo kutokana na mafanikio aliyoyapata kwa muda mfupi ndani ya Chelsea toka ajiunge nayo msimu juzi. Amewahi kufundisha vilabu mbalimbali vikiwemo Borrusia Dortmund, Psg na zinginezo.

Toka aichukue klabu hiyo ambayo ilikuwa chini ya kocha Frank Lampard alicheza michezo 100 na kushinda michezo 60, sare zikiwa 24 na kupoteza michezo 16 peke yake huku magoli ya kufunga yakiwa 168, na akiruhusu nyavu zake kutikiswa mara 77.

 

Tuchel 49 Avunja Ukimya

Thomas ambae ni raia wa Ujerumani ndani ya huo mfupi ameweza kuipatia Chelsea mataji mbalimbali ikiwemo taji la UEFA msimu juzi, kombe la mabingwa barani Ulaya na kombe la Super Cup, Lakini kutokana na klabu hiyo kutumia pesa nyingi kwenye usajili na kushindwa juwa na matokeo mazuri uwanjani kumefanya kibarua chake kiote nyasi na kutimuliwa baada ya kuanza vibaya kwenye ligi na kupoteza mechi ya kwanza ya UEFA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa