Kocha wa klabu ya Chelsea Thomas Tuchel ameweka wazi umuhimu wa kumpa muda nyota wake mpya aliiyemsajiri kutokea klabu ya Inter milan Cesare Casadei ili kuweza kupata muda wa kuzoea na kutulia kwenye viunga vya Stamford Bridge.

Cesare Casadei amesajiri kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kwenye uhamisho ulioyoigharimu kiasi cha €20milioni akitokea klabu ya Inter Milan kwenye kikosi cha chini ya miaka 19 msimu uliopita.

Thomas Tuchel, Thomas Tuchel: Sina Haraka na Cesare Casadei, Meridianbet

“Tunahitaji kumpa muda na sio kumfurahia zaidi kwa sababu hiyo haitamsaidia yeye,” aliuwambia mtandao wa Chelsea Thomas Tuchel.

“Yeye ni kiungo anayecheza ‘box-to-box’ imara sana kichwani, ananguvu kwa umri wake lakini kwa kipindi hiki ni muhimu ajifunze lugha, ajifunze na Chelsea inahusu nini na kuielewa tamaduni yake na misingi ya kuishi na kuichezea Chelsea.

“Kisha tutajaribu kumuingiza kwenye mazoezi na timu ya wakubwa na kumfungulia milango, mwishowe , atahitaji apige hatua yeye mwenyewe.”

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa