LICHA ya ligi kusimama ili kupisha michezo ya kimataifa ambapo timu ya Taifa ya Tanzania ikicheza dhidi ya Uganda lakini kikosi cha Singida Big Stars kimetimkia Arusha kwa ajili ya kujifua.

Katika michezo miwili ya ligi waliyocheza Singida Big Stars wamefanikiwa kukusanya pointi zote sita wakikipiga dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons.

Singida Big Stars, Singida Big Stars Hakuna Kulala, Meridianbet

Akizungumzia hilo, Mkurugenzi wa masoko na fedha wa Singida Big Stars, Muhibu Kanu amesema kuwa: “Kwanza tunamshukuru Mungu kikosi chetu kipo salama na hakuna mchezaji yeyote ambaye ameondoka kambini wote wapo.

“Kikosi kiliondoka jana usiku hapa Singida kuelekea Arusha ambapo tutaweka kambi huko kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya ligi kuu inayofuata.

“Kuhusu mchezaji wetu Dario Frederico niwatoe wasiwasi wana Singida kuwa huyo bado ni mchezaji wetu haendi popote kwani tuna mkataba naye wa miaka mitatu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa