Mcheza Tenisi wa Hispania, Carlos Alcaraz, 19 ameshinda taji lake la kwanza la Grand Slam kwenye mashinjdano ya US Open Jumapili usiku na kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kushika nafasi ya kwanza duniani.

 

Alcaraz 19 Ashinda Grand Slam

 

Alcaraz alichuana fainali ya US Open dhidi ya Casper Ruud katika Uwanja wa Arthur Ashe wakiwania taji la kwanza la Grand Slam na kuibuka mshindi kwa seti 6-4 2-6 7-6 (7-1) 6-3.

Carlos Alcaraz amevunja rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kutwaa ubingw awa US Open akimshinda Lleyton Hewitt aliyefanya hivyo mwaka 2001 akiwa mkubwa kwa mwaka mmoja zaidi.

 

Alcaraz 19 Ashinda Grand Slam

“Hili ni jambo nililolitamani tangu nikiwa mtoto mdogo. Kuwa namba moja duniani, na kuwa bingwa wa Grand Slam,” alisema Alcaraz.

“Jitihada zote ngumu nilizofanya na timu yangu, familia yangu. Nina umri wa miaka 19 tu hivyo maamuzi mengi yapo kwa timu yangu, wazazi wangu. Ni kitu cha kipekee sana kwangu.”

Mchezaji huyo alikiri kwa tabasamu kwamba alikuwa amechoka “kidogo”, lakini alisema: “Mara nyingi nimekuwa nikisema sio wakati wa kuchoka katika raundi ya mwisho ya Grand Slam. Unapaswa kutoa kila kitu uwanjani, kila kitu ulichonacho.”

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa