Jurgen Klopp ana uhakika kuwa Nunez ataanza kufunga hivi karibuni baada ya utendaji wake “wa kipekee” katika ushindi wa Siku ya jana walipokuw wakicheza dhidi ya Aston Villa.

Mohamed Salah, Virgil van Dijk na Stefan Bajcetic walipata bao lao huku Liverpool ikirejea kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza kwa ushindi wa 3-1 kwenye uwanja wa Villa Park, ambapo Nunez alionyesha kiwango kizuri.
Nunez aliwaongoza wachezaji wote uwanjani kupiga mashuti (sita), kujaribu kulenga shabaha nne kwenye eneo la wapinzani, wakati baadhi ya watu wakimkosoa Nunez kwa kutokuwa na msimamo mbele ya lango, Klopp hana wasiwasi wowote kuhusu maendeleo ya Mruguay huyo.
Klopp aliiambia Amazon Prime Video kuwa inashangaza alicheza mchezo gani, bila shaka atafunga. “Nilikuwa katika hali hii mara nyingi sana na washambuliaji, na kila kitu kitakuwa sawa mchezo wake ulikuwa wa kipekee.”

Liverpool sasa wameshinda mechi tatu mfululizo za Primia Ligi kwa mara ya kwanza msimu huu, na Klopp alifurahishwa na uwezo wao wa kuhimili shinikizo kali kutoka kwa wenyeji.
“Ilikuwa kiwango cha juu katika mchezo mgumu, tulicheza kipekee katika kipindi cha kwanza, ingawa Villa walikuwa na wakati wao. Tulikuwa wazuri sana, nilipenda nilichokiona.”
Klopp aliongeza kwa kusema kuwa kipindi cha pili walikosa hatua ya mwisho kidogo, na Aston Villa walikuwa wakija kwa nguvu hiyo ni kawaida katika mchezo wa nyumbani na walijua hilo lingetokea.

Akizungumza na tovuti rasmi ya klabu hiyo, Robertson alikiri kuwa amekuwa akiitazama rekodi hiyo katika kipindi chote cha mapumziko ya Kombe la Dunia.
Roberson amesmea kuwa, beki wa pembeni amebadilika sana na inahusu kwenda mbele sasa na pia kulinda. Lakini kwanza kabisa, anataka kujilinda na mambo kama hayo lakini ni sehemu kubwa ya mchezo wao.

