Casemiro: Anaweza Kua Miongoni mwa Wachezaji Watano Bora Duniani

Kiungo wa shoka wa klabu ya Manchester United Carlos Casemiro amesema kua mchezaji mwenzake wa klabu hiyo Marcus Rashford anaweza kua miongoni mwa wachezaji bora watano duniani.

Marcus Rashford alianzia nje katika mchezo dhidi ya Wolves baada ya kulala na kushindwa kuhudhudria kikao kabla ya mchezo, Lakini mchezaji huyo alitokea nje na kufunga bao pekee lililoipa Manchester United alama tatu muhimu dhidi ya Wolves.casemiroMshambuliaji Marcus Rashford mpaka sasa ameshafunga mabao 11 kwenye michezo 22 aliyocheza na kuonesha kuimarika zaidi chini ya kocha Ten Hag, Kwani msimu ulimalizika mchezaji huyo alifunga mabao matano pekee msimu mzima.

Kiungo Casemiro alipoulizwa kuhusu mchezaji huyo mwenzake alisema “Niwe mkweli nilishangazwa na Rashford, Kwa maoni yangu haswa nikimjua mchezaji nje ya Uwanja, Kama ataendelea hivi anaweza kua miongoni mwa wachezaji watano bora duniani”casemiroMarcus Rashford amekua na msimu bora sana kwenye kikosi cha Manchester United na kua miongoni mwa wachezaji tegemezi ndani ya timu hiyo, Jambo lililomfanya Casemiro kuamini mchezaji huyo akiendeleza ubora wake atakua moja ya wachezaji watano bora duniani.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.