Vinara wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Arsenal na Manchester United zatawala katika tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa ligi kuu ya Uingereza kwa mwezi Novemba na Disemba.
Klabu ya Arsenal na Man United zimefanikiwa kuttoa wachezaji wawili wanaogombea tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Novemba na Disemba ambazo zimechanganywa kwa pamoja, Klabu hizo zimetoa wachezaji wanne kwa ujumla wawili kila timu.
Klabu ya Arsenal imefanikiwa kuwaingiza Martin Odegaard na Bukayo Saka huku klabu ya Man United wao wamewaingiza kiungo Carlos Casemiro pamoja mshambuliaji Marcus Rashford, Timu hizo mbili ndio zimefanikiwa kutoa wachezaji wawili kwenye tuzo hizo huku klabu zingine ziktoa mchezaji mmoja tu.
Tuzo hiyo itawaniwa na wachezaji nane huku vilabu hivo viwili vikitoa wachezaji wanne pekee. Vilabu vingine vilivyofanikiwa kutoa wachezaji kuwania tuzo hiyo ni Fulham iliyomtoa Joao Palhinha, Manchester City wao wamewakilisha na Haaland, klabu ya Newcastle wao ni beki Kieran Treppier, na klabu ya Southhampton wao wakiwakilishwa na James Ward Prowse.
Wachezaji hao nane wameonekana kua kwenye ubora mkubwa ndani ya miezi miwli iliyopita na ndio sababu ya wao kua kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, Tuzo hiyo inatarajiwa kutolewa mapema Januari hii.

