Van De Beek Nje Msimu Mzima

Kiungo wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uholanzi Donny Van De Beek anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu kilichobakia.

Kiungo huyo Van De Beek ambaye alipata majeraha katika mchez dhidi ya Bournamouth na kutolewa nje ya uwanja baada ya kuchezewa rafu mbaya, Taarifa iliyotoka rasmi kupitia kocha Erik Ten Hag mchezaji huyo atakua nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu kilichobakia.van de beekKiungo huyo amekua akipitia kipindi kigumu ndani ya klabu hiyo toka alipojiunga hapo akitokea klabu ya Ajax, Kiungo huyo amekua akikosa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza ndani ya kikosi cha Manchester United.

Donny Van De Beek vilevile ameandamwa na majeruhi kwa kiwango kikubwa sana tangu ajiunge na mashetani wekundu, Kwani kabla ya kupata majeruhi dhidi ya Bournamouth wiki kadhaa nyuma alikua ametoka kupona majeraha ambayo yalimueka nje ya kiwanja kwa muda kidogo.van de beekKiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi anaweza kujiona asiye na bahati ndani ya Manchester United kwani kipindi hichi ambacho alikua fiti ndio wakati amba alianza kupewa nafasi na kocha Erik Ten Hag, Lakini muda mfupi tu mchezaji huyo amepata majeraha makubwa yanayomueka nje ya uwanja mpaka msimu ujao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.