Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola anatarajiwa kufikisha mchezo wake wa 500 kama kocha katika mchezo wa Manchester Derby utakaopigwa kesho jumamosi.
Kocha huyo ambaye atafikisha mchezo wa 500 hapo kesho kati ya timu yake na mahasimu wao klabu ya Manchester United mchezo utakaopigw katika dimba la Old Trafford. Mchezo huo ambao unatarajiwa kua wenye ushindani mkubwa zaidi.
Itakua mechi muhimu kwa kocha Pep Guardiola kufikisha mchezo wake wa 500 kama kocha na atahitaji kumaliza rekodi hiyo kwa ushindi , Klabu ya Manchester City ikifanikiwa kupata matokeo ya ushindi katika mchezo wa kesho itakua mchezo wa nne mfululizo wanapata matokeo dhidi ya mahasimu wao hao.
Mchezo wa kati ya Manchester City dhidi ya Man United unatarajiw akua mchezo mgumu zaidi kuliko michezo yote waliyocheza kwa miaka ya karibuni, Na hii ni kutokana na hali ya timu zote mbili huku City wao wakihitaji kupunguza pengo la alama ili kuwakaribia vinara Arsenal na United wao wakiwa kwenye kiwango bora kabisa.
Klabu ya Manchester United mpaka sasa imefanikiwa kushinda michezo nane mfululizo huku Manchester City chini Pep Guardiola wao wakiwa wametoka kupoteza mchezo kabla ya kwenda kumenyana na mahasimu wao klabu ya Man United. Kiuhalisia mchezo huo unatarajiwa kua mgumu lakini wenye mvuto mkubwa.

