Simba na Yanga imesajili wachezaji 4 kila mmoja | Waliosajiliwa na Simba Ismael Sawadogo (Kiungo wa Ulinzi-Mkata umeme), Saido Ntibazonkiza (Winga) Jean Baleke (Straika) na Mohammed Mussa (Straika) | Yanga ni Mudathir Yahya (Kiungo) Kennedy Musonda (Straika), Mamadou Doumbia (Beki wa kati) na Metacha Mnata (Mlinda mlango).

Simba na Yanga: Dirisha la usajili limefungwa rasimi huku tukishuhudia vilabu vya Ligi kuu ya NBC vikisajili ili kujiimarisha zaidi kabla ya Ligi kuisha. Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet.
Timu kubwa za Tanzania Simba na Yanga zimemaliza usajili huku kila moja ikitambulisha wachezaji wao ambao waytaungana na wenzao kuanza maandalizi ya mechi za ndani na za kimataifa.
Yanga imesajili jumla ya wachezaji 4, Mudathir Yahya (Kiungo) Kennedy Musonda (Straika), Mamadou Doumbia (Beki wa kati) na Metacha Mnata (Mlinda mlango). Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kubashiri.

Usajili huu kwa upande wa kuongeza upana wa kikosi ni sawa kwa asilimia 100% lakini kwa upande wa kiufundi na mahitaji ya timu Yanga wamefanikiwa kwa asilimia 60%
Ukiangalia maeneo ambayo yamesajiliwa ni tayari yalikuwa na watu sahihi tu kama Makambo upande wa ushambuliaji, beki ya kati kuna Job, Mwamnyeto na Yannick Bangala, pia kuna Ibrahim Bacca, lakini bado wameleta Doumbia labda kwa sababu za Kimataifa.
Walinda mlango wanao watatu mpaka sasa, Namba moja ni Diara, Mshery na Johora lakini bado kaja Metacha kuongeza nguvu huu sidhani kama ni usajili wenye uhiataji kwa sasa kwa Yanga. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii!!.
Lakini ukija kwa watani zao Simba tangu kuanza kwa msimu huu tatizo kubwa lkilikuwa ni eneo la kiungo na mshambuliaji hatari, Simba wamewasajili wachezaji 4 pia kama Yanga, Ismael Sawadogo (Kiungo wa Ulinzi-Mkata umeme), Saido Ntibazonkiza (Winga) Jean Baleke (Straika) na Mohammed Mussa (Straika).

Kidogo kwa Simba unaweza kuona wamesajili kulingana na mahitaji ya timu kwa muda muafaka, walikuwa na shida ya mkata umeme wamesajili Sawadogo, pia walikuwa na tatizo la namba 9 asilia wamemleta Jeam Baleke kutoka TP Mazembe ambaye alikuwa ni mshindani mkubwa na Fiston Mayele wa Yanga. Pata Odds kubwa za soka ukiwa na Meridianbet.
Simba na Yanga wote wana mechi za kimataifa ambazo zinatarajia kuanza mapema mwezi wa 2, 2023, Yanga akishiriki mashindano ya Shirikisho barani Afrika huku Simba wakiwa upande wa Ligi ya Mabingwa(CCL) usajili huu utawasaidia kwa kiasi gani kwenye mashindano ya ndani na Kimataifa?

