Simba Yaanza Kurejea Leo Kutoka Dubai

Baada ya kukaa Dubai kwa wiki moja, rasmi sasa Simba wameanza safari ya kurejea Dar es salaam hii leo kujiandaa na mchezo wao wa kesho dhidi ya Mbeya City.

 

Simba Yaanza Kurejea Leo Kutoka Dubai

Simba walicheza mechi mbili za kirafiki walipokuwa Dubai ambapo mechi ya kwanza walimenyana dhidi ya AL Dhafra na wakapoteza kwa bao 1-0, huku mechi ya pili wakicheza dhidi ya CSKA Moscow ya Urus na kutoa sare ya kufungana 2-2.

Katika mchezo huo dhidi ya CSKA Moscow ni Habib Kyombo amabe aliisawazishia Lunyasi mabao hayo ambayo tayari walikuwa wameshafungwa na timu hiyo yenye historia kubwa Duniani.

Simba Yaanza Kurejea Leo Kutoka Dubai

Mchezo wao na Mbeya City unatarajiwa kupigw akatika Dimba la Benjamin Mkapa saa 1:00 usiku huku mechi ya kwanza kukutana mnyama alilazimishwa sare ya 1-1 akiwa ugenini.

Mbeya City wapo nafasi ya 10 baada ya kucheza michezo yao 19 wakiwa wamejikusanyia pointi zao 21, huku Simba wao wapo nafasi yao ya pili wakiwa na pointi zao 44 na mchezo wa kesho watahitaji ushindi kupunguza gepu lililopo kati yao na watani zao Yanga.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.