Klabu ya Azam FC yaendeleza ushindi wake wa pili mfululizo baada ya kuichapa bakora tatu nunge timu ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wao wa raundi ya 20 uliopigwa majira ya saa 2:30 usiku Chamazi.

Mabao hayo ya Azam yalitupiwa kimyani na Prince Dube, Sopu pamoja na Kipre Junior katika vipindi vyote vya mchezo huku Sopu akiendeleza kupachika mabao kwenye kila michezo ya hivi karibuni.
Baada ya ushindi huo sasa vijana wa Kally Ongala wamebaki nafasi yao ile ile ya tatu kwenye msimamo wakiwa wamekusanya pointi zao 43 baada ya michezo 20 waliyocheza huku Wajela jela wakiwa na pointi zao 21.

Tanzania Prisons wamepoteza mechi mbili mfululizo kwenye ligi hadi sasa na mchezo unaofuata watamenyana dhidi ya Ihefu ambao nao wametoka kupoteza mchezo wao wa jana.
Kituo kinachofuata kwa Azam ni dhidi ya Singida Big Stars ugenini, ambao wapo nafasi ya nne na wanatarajia kukipiga leo dhidi ya Kagera Sugar.

