Mayele Aitafuna Ihefu kwa Mkapa

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele ameitafuna Ihefu bao 1-0 katika mchezo wao wa jana uliopigwa majira ya saa 12:30 katika dimba la Benjamin Mkapa.

 

Mayele Aitafuna Ihefu kwa Mkapa

Bao hilo la Mayele alilifunga katika kipindi cha pili cha mchezo baada ya dakika 45 za kwanza za mchezo kumalizika bila kufungana, ndipo waliporejea kipindi cha pili na mshambuliaji huyo hatari kupachika bao hilo dakika ya 64.

Mshambuliaji huyo ambaye sasa amefikisha mabao 15, alitumia makosa ya mlinda mlango wa Ihefu Mapara baada ya kupiga vibaya huku golini kukiwa hamna ndipo shughuli yao ilipoishia hapo kwani ndilo bao lililosalia mpaka dakika za mwisho za mchezo.

Hivyo mpaka sasa Yanga wamefikisha pointi zao 53 baada ya kucheza michezo 20 wakiwa wamelipa kisasi cha kufungwa mechi ya kwanza na timu hiyo kutoka Mbeya.

Mayele Aitafuna Ihefu kwa Mkapa

Baada ya kupoteza mchezo huo klabu ya Ihefu wamezidi kusalia katika nafasi ya 13 ambayo sio salama kama wakiendelea hivyo mpaka mwisho wa msimu na ligi bado ina ushindani. Mlinda mlango wao amefanya kosa la kuigharimu timu yao huenda wangeambulia sare.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.