Guardiola: Muhimu Kushinda Mchezo Unaofuata

Kocha wa Klabu ya Manchester City Pep Guardiola ameweka wazi kua kipaumbele chake kwasasa zaidi ni kushinda mchezo ambao upo mbele yao zaidi ya kuangalia yaliyopita.

Klabu ya Manchester City ilipotezxa mchezo wake siku ya jumamosi dhidi ya mahasimu wao klabu ya Manchester United katika mchezo wa Manchester Derby. Kitu ambacho Guardiola anaamini sio cha kukiangalia kwasasa zaidi ni kuangalia zaidi mchezo ambao upo mbele yao.guardiolaKocha huyo ameeleza kua siku zote unatakiwa kuzingatia mchezo unaofuata zaidi kuliko mchezo ambao tayari umepita, Kwani mchezo ambao umepita anaamini hauwezi kwenda kubadilisha chochote zaidi unahitaji kuangalia unapata matokeo vipi katika michezo inayofuata.

Pep Guardiola pia amepinga kua klabu hiyo inapata tabu kuendana na aina ya uchezaji wa mshambuliaji wao hatari Earling Haaland, Na kuweka wazi timu hiyo inacheza vizuri ikiwa na mshambuliaji huyo na wala hakuna changamoto yeyote kwani bado wanatengeneza nafasi vizuri.guardiolaKlabu ya Manchester City inatarjiwa kukipiga dhidi ya klabu ya Tottenham Hotspurs katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza siku ya Alhamisi, Huku timu zote mbili zikiwa zimetoka kupoteza katika michezo yao iliyopita hivo unatarajiwa kua mchezo mgumu zaidi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.