Mshambuliaji wa klabu ya Fc Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi Memphis Depay yuko katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Atletico Madrid.
Memphis Depay ambaye amekua akikosa nafasi ndani ya klabu ya Barcelona amefikia katika hatua za mwisho za kujiunga na klabu ya Atletico Madrid. Mchezaji huyo ameamua kuondoka timu hiyo ili kwenda kupata nafasi ya kucheza ambayo ameikosa ndani ya Barcelona.
Mshambuliaji huyo ameripotiwa kujiunga na klabu ya Atletico Madrid kwa uhamisho wa jumla tofauti na ambavyo iliripotiwa mwanzo kua mchezaji huyo angejiunga kwa mkopo, Lakini mchezaji huyo atakwenda kwenye klabu ya Atletico kwa uhamisho wa kudumu.
Kocha Xavi alizungumza leo kua anatarajia kuzungumza na mchezaji huyo kuhusu mpango wake wa kuondoka klabuni hapo, Lakini taarifa ambazo zimefika jioni ya leo ni kua mchezaji huyo ataelekea klabu ya Atletico Madrid kwa uhamisho wa kudumu.
Memphis Depay ambaye alikua anahitajika na vilabu mbalimbali vya nchini Uingereza ikiwemo klabu ya Manchester United, Lakini mchezaji huyo ameamua kujiunga na Atletico de Madrid kutokana na vipaumbele alivyovizingatia mchezaji huyo mojawapo ni kupata nafasi ya kucheza.

