Bruno Fernandes Kuweka Rekodi Leo

Kiungo wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes leo anaweza kuweka rekodi katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Crystal Palace.

Bruno Fernandes amekua kwenye kiwango bora sana tangu amejiunga na klabu ya Manchester United mwaka 2020, Mchezaji huyo amefanikiwa kuhusika kwenye magoli 99 tangu ajiunge ndani ya timu hiyo mwaka 2020 na leo akifunga bao au kupiga pasi ya bao anaenda kuweka rekodi.bruno fernandesKiungo huyo ameshafunga magoli 54 na kupiga pasi 54 za mabao tangu ajiunge kwenye klabu ya Manchester United hivo kumfanya ahusike kwenye mabao 99, Mchezaji huyo anasubiriwa atengeneze pasi ya bao au afunge katika mchezo huo ili aweze kuhusika kwenye mabao 100 ndani ya klabu hiyo.

Bruno Fernandes ni kiungo ambaye amekua na takwimu nzuri ndani ya ligi kuu ya Uingereza huku akiwa anashikilia usukani kwenye viungo wanaoongoza kwa kutengeneza nafasi kwenye ligi hiyo tangu ajiunge na klabu ya Manchester United .bruno fernandesKiungo huyo ambaye amesaini kandarasi mpya mapema kabla ya kuanza kwa msimu huu amekua moja ya wachezaji muhimu zaidi ndani ya klabu hiyo, Na hiyo ni kutokana na mchango mkubwa ambao amekua nao ndani ya klabu ya Manchester United.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.