Unazijua Timu Zilizopewa Penati Nyingi Mpaka Sasa? Hizi Hapa

Baada ya mzunguko wa 20 wa Ligi kuu ya NBC kumalizika hizi hapa ndio timu ambazo zimeongoza kwa kupewa penati nyingi kuliko zingine huku zingine zikipata zote na zingine kukosa baadhi.

 

Unazijua Timu Zilizopewa Penati Nyingi Mpaka Sasa? Hizi Hapa

Timu ya kwanza ni Dodoma Jiji kutoka kule Makao makuu ya nchi ambao wao mpaka sasa kwenye michezo yao 20 waliyocheza wamepata penati 6, lakini cha kushangaza ni penati moja tu waliyopata zote tano wamekosa. Wapo nafasi ya 12 pointi 21.

Timu ya pili ni Geita Gold ya Felix Minziro huku wao wakiwa wamepata penati nne, katika hizo penati wamefanikiwa kutupia kambani zote. Mpaka sasa wapo nafasi ya 5 wakiwa na pointi zao 27.

Klabu nyingine iliyopo kwenye msururu wa penati ni Tanzania Prisons ambao nao ni kama Geita wamepata penati 4 na wamefanikiwa kuzifunga zote kambani. Wapo nafasi ya 11 wakivuna pointi 21.

Unazijua Timu Zilizopewa Penati Nyingi Mpaka Sasa? Hizi Hapa

Singida Big Stars inaongozana na timu hizo mbili za juu, amabpo vijana hawa wa Hans Pluijm nao wamepata mikwaju ya penati minne, wakipata mitatu na kukosa moja, wakishikilia nafasi ya 4 pointi 40.

Mabingwa watetezi wa Ligi Yanga wao pia wamepata penati 3, na wamekosa mbili kati ya hizo wakipata moja. Nafasi ya kwanza kwenye msimamo wakivuna pointi zao 53 wakiwa mbele pointi sita kwa anayemfuata.

Unazijua Timu Zilizopewa Penati Nyingi Mpaka Sasa? Hizi Hapa

Na timu ya mwisho ni Ruvu Shooting ambao nao pia wamepata penati 3, lakini iliyoingia nyavuni ni moja pekee, huku mbili wakizikosa. Nafasi ya 15 wanashikilia ambayo ni ya pili kutoka mwisho baada ya kuvuna pointi 14.

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.