Klabu ya Simba inaelezwa inamfukuzia kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah ambaye inaelezwa wanamhitaji aje kua mkurugenzi wa ufundi klabuni hapo.
Klabu ya Simba imepanga kua mkurugenzi wa kiufundi kwa mara ya kwanza klabuni hapo ambapo atakua ana majukumu tofauti kidogo na ya mkurugenzi wa timu, Kwani mkurugenzi wa ufundi atakua kwenye nafasi nzuri zaidi ya kua karibu na timu na kusimamia kila kitu kinachoihusu timu.
Wekundu wa Msimbazi walikua wanamfukuzia kocha huyo wa zamani wa Ghana kwa muda mrefu kwani inaelezwa kabla ya klabu hiyo kumuajiri Zoran Maki ambaye alitimkia nchini Misri baadae walimuhitaji kocha huyo, Lakini haikuwezekana hivo klabu hiyo imerudi tena kuhakikisha wanapata saini ya gwiji huyo kama mkurugenzi wa klabu hiyo.
Taarifa kutoka nchini Ghana zinaeleza kocha Kwesi Appiah atajiunga na klabu ya Simba kama ikitokea amekosa nafasi ya kua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah ameomba nafasi ya kua kocha mkuu wa klabu hiyo hivo akikosa nafasi hiyo basi wekundu wa msimbazi watampata gwiji huyo.

