Klabu ya Manchester United imemgeukia kiungo wa klabu ya Fc Bayern Munich Marcel Sabitzer ambaye inaeklezwa anakuja kuziba pengo la Christian Eriksen.
Klabu ya Manchester United ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Fc Bayern Munich ili kumpata kiungo huyo kwenye siku ya mwisho kabisa ya usajili barani ulaya, Klabu hiyo ipo kwenye mkakati huo ambao imekua ghafla kwao kutokana na majeraha yaliyoibuka ghafla kwenye klabu hiyo.
Klabu hiyo inataka kuharakisha dili hilo kutokana na taarifa zilizotoka leo kutoka klabuni hapo kua kiungo wao Christian Eriksen atakosekana kwenye timu mpaka mwezi wa nne mwishoni au mwezi wa tano mwanzoni, Hivo klabu hiyo wanahitaji mbadala wa kiungo huyo haraka iwezekanavyo.
Kiungo Marcel Sabitzer inaelezwa ameomba kuondoka ndani ya klabu ya Bayern Munich na anavutiwa zaidi na kujiunga na klabu ya Man United, Taarifa kutoka Ujerumani zinaeleza kiungo huyo amemalizana na United na kilichobaki ni Bayern kumruhusu aondoke.
Dirisha dogo la usajili linafungwa usiku wa leo saa sita kwa majira ya ukanda wa Afrika Mashariki na klabu ya Manchester United inapambana kuhakikisha kwa kiwango kikubwa kua dili hilo linakamilika mapema kabla ya dirisha kufungwa, Kwani itakua changamoto kwao kupata mbadala wa Eriksen.

