Manchester United Wanafikiria Kuingia Sokoni Kwajili ya Eriksen

Taarifa zinaeleza kua klabu ya Manchester United inafikiria kuingia sokoni kutafuta kiungo kutokana na majeraha ambayo amepata kiungo fundi Christian Eriksen katika mchezo wao dhidi ya Reading.

Manchester United ilikua haina mpango wa kusajili kiungo katika dirisha dogo la mwezi Januari lakini kutokana na majeraha ambayo amepata kiungo wao, Ni wazi wameanza kufikiria namna wanaweza kuingia sokoni na kupata kiungo ambae anaweza kuja kuvaa viatu vya Eriksen.manchester unitedKiungo Christian Eriksen amekua moja ya wachezaji muhimu katikati mwa kiwanja kwenye klabu ya Man United akishirikiana na wachezaji kama Casemiro, Bruno Fernandes, na Fred hivo kupata kwake majeraha kunampasua kichwa kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag kutokana na umuhimu ambao amekua nao kwenye kikosi hicho.

Klabu ya Manchester United ina viungo ambao inawaangalia kwa jicho la karibu ndani ya dirisha hili ambao wanaweza kuchukua nafasi ya Eriksen ambaye haijafahamika atarudi lini kiwanjani, Youri Tielemans kutoka klabu ya Leicester City ni kiungo anaefatiliwa kwa karibu na mashetani hao wekundu.manchester unitedManchester United mpaka sasa ipo kwenye michuano yote hivo wanahitaji kikosi kipana cha kuweza kupambana katika michuano hiyo, Hivo kuumia kwa kiungo huyo ni wazi kumepunguza nguvu kikosini sasa klabu hiyo inataka kuingia sokoni kutafuta kiungo mwenye ubora ili waendelee kua na nguvu kwenye michuano ambayo wanashiriki.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.