Klabu ya Ajax imeonekana kufufuka kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uholanzi leo baada ya kupata ushindi wa mabao manne kwa moja dhidi ya klabu ya Excelsior.
Klabu hiyo ambayo imemfukuza kocha wake wiki iliyomalizika kutokana na mfululizo wa matokjeo mabaya ambayo amekua akiyapata klabuni hapo siku za hivi karibuni. Klabu ya Ajax leo imeweza kupata ushindi wa kwanza toka waachane na kocha wao wa zamani.
Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Uholanzi wanapitia kipindi kigumu kwasasa ambapo walikua hawajapata matokeo ya ushindi katika michezo mitatu ya hivi karibuni, Lakini leo kw amara ya kwanza wamepata matokeo ya ushindi chini ya kocha wa muda klabuni hapo John Heitinga.
Ajax wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uholanzi mpaka sasa hii inaonesha kua klabu hiyo inapitia kipindi kigumu ndani ya msimu huu, Kwani klabu hiyo kwa takribani misimu minne au mitatu ya hivi karibuni imekua ikifanya vizuri na wakati kama huu ilikua unaikuta kileleni mwa msimamo au nafasi ya pili lakini msimu huu mambo yamekua tofauti.
Kuondoka kwa kocha wao ambaye amewapa mafanikio miaka ya karibuni Erik Ten Hag ambaye alitimkia klabu ya Manchester United inaelezwa kua ni sababu ya klabu hiyo kuweza kutetereka msimu huu, Lakini pia klabu ya Ajax iliweza kuachia wachezaji wake nyota ndani ya kikosi hicho bila kuziba nafasi zao na wachezaji wenye ubora mkubwa.

