Tanzania Ligi bora namba Tano Afrika

Ligi kuu ya soka Tanzania imefanikiwa kushika nafasi ya tano katika viwango vya ubora Barani Afrika hii imeripotiwa na shirikisho la kimataifa la historia na takwimu za mpira wa miguu linalojulikana kama (IFFHS).

Ligi kuu ya Tanzania imefanikiwa kukamata nafasi ya tano kwenye ubora wa ligi barani huku wakiwa nyuma ya mataifa makubwa kama Misri inayokamata nafasi ya kwanza, Algeria nafasi ya pili, Morocco wakikamata nafasi ya tatu huku nafasi ya nne wakishika Sudan.

Ligi ya Tanzania Bara imefanikiwa kukua kwa kiwango kikubwa ndani ya miaka ya karibuni, Huku vilabu vya nchini Tanzania pia vikifanikiwa kufika katika hatua kubwa katika ligi ya mabingwa Afrika pamoja na ile ya kombe la shirikisho barani Afrika.Kufanya vizuri kwa vilabu vya hapa nchini imekua chachu ya kukua kwa ligi ya hapa kutokana na kutambulika katika sehemu mbalimbali kumesaidia kwa kiwango kikubwa kukua kwa ligi. Kwasasa ligi ya hapa nchini imeendelea kukua na kupanda thamani kila uchwao.

Ligi ya hapa nchini imekamata nafasi ya tano ndani ya bara la Afrika ikiwa inaonesha maendeleo makubwa ya mpira hapa nchini, Lakini pia imeweza kukamata nafasi ya 39 kwa ubora duniani ikiwa pia ni mafanikio makubwa sana ndani ya soka la Tanzania.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.