Ten Hag: Nataka Mabeki Wangu wa Kati Wacheze kama Viungo

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amesema anapenda mabeki wake wa katikati wacheze kama viungo katika timu yake akizungumza baada ya kumchezesha beki wake Lindelof kama kiungo wa ulinzi.

Kocha Ten Hag jana alimchezesha beki Victor Lindelof katika nafasi ya kiungo wa ulinzi katika mchezo wa jana wa kombe la Carabao hatua ya Nusu Fainali, Hiyo ni baada ya beki huyo kutoka benchi akichukua nafasi ya kiungo wa ulinzi wa timu hiyo Carlos Casemiro.Ten HagKocha huyo wakati akizungumza na wanahabari alisema kua beki wake Lindelof wakati yupo klabu ya Benfica alifundishwa kucheza kama namba 6 hivo anaamini anaweza kucheza nafasi hiyo, Pia akisema anahitaji mabeki wake wacheze katika nafasi hiyo ili kutengeneza mabadiliko katika kikosi chake.

Beki Victor Lindelof amekua akikosa nafasi ya kuanza mara kwa mara kwenye kikosi cha Manchester United, Hivo kocha Ten Hag ili kuwapatia nafasi baadhi ya mabeki wake na kuwachezesha katika nafasi ya kiungo wa ulinzi.Ten HagKocha Erik Ten Hag pia ameeleza kufurahishwa na klabu yake kuweza kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Carabao mwishoni mwa mwezi huu, Huku klabu ya Manchester United wakiwa na nafasi ya kubeba taji lao la kwanza baada ya miaka takribani mitano.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.