Klabu ya Real Madrid itashuka dimbani leo katika mchezo wa nusu fainali wa klabu bingwa ya dunia dhidi ya klabu ya Al Ahly utakaopigwa nchini Morocco katika dimba la Pince Moulay Abdellah.
Klabu ya Real Madrid ambao wanaliwakilisha bara ulaya baada ya kutwaa taji la ligi ya mabingwa ulaya msimu uliomalizika, Hivo leo watamenyana na klabu ya soka ya Al Ahly kutoka nchini Misri wao wakiliwakilisha bara la Afrika.
Los Blancos leo wanashuka dimbani kuhakikisha wanakwenda fainali ili kwenda kulisaka taji la tano la klabu bingwa ya dunia na kuendelea kua kinara wa kombe hilo, Mpaka sasa mabingwa hao watetezi wa ligi ya mabingwa ulaya wameshashinda taji hilo mara nne wakiwa ndo vinara wakifanya hivo mwaka 2014,2016,2017, na 2018.
Real Madrid wamekua hawapo kwenye ubora wao ambao walianza nao msimu huu punde tu baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia, Jambo ambalo limewapa hofu mashabiki wa klabu hiyo huenda wakakosa taji hilo kwa mara ya kwanza.
Klabu ya Real Madrid itaendelea kumkosa mshambuliaji wake namba moja Karim Benzema ambae bado anasumbuliwa na majeraha, Lakini nyota wengine muhimu ndani ya kikosi hicho wapo kuhakikisha klabu hiyo inaendeleza rekodi yake bora kwenye michuano hiyo.

