Klabu ya Real Madrid inaelezwa haina mpango wa kumfukuza kocha wake ndani ya klabu hiyo Carlo Ancelotti kama ambavyo vyanzo tofauti vinaeleza.
Taarifa mbalimbali zinaeleza kua klabu ya Real Madrid ina mpango wa kumfukuza kazi kocha wake kutokana na muendelezo mbaya wa matokeo ndani ya klabu hiyo, Lakini vyanzo kutoka ndani ya klabu hiyo vinaeleza kua klabu ya Real Madrid haina mpango wa kumfukuza kocha Ancelotti.
Klabu hiyo kwasasa imekua kwenye wakati mgumu kutokana na matokeo ambayo imekua ikiyapata ndani ya msimu huu, Kutokana na muenendo wa klabu hiyo imesababisha kuibuka kwa uvumi kua kocha huyo huenda akaondolewa ndani ya klabu hiyo.
Taarifa zimeenda mbali zaidi na kudai kua kama klabu ya Real Madrid itashindwa kutwaa taji la klabu bingwa ya dunia basi huenda kocha Ancelotti akafukuzwa ndani ya timu hiyo, Lakini msimamo wa klabu hiyo bado upo palepale kua bado wana mpango kuendelea na kocha huyo.
Klabu ya Real Madrid kwasasa inashiriki kwenye michuano ya kombe la dunia ambayo inafanyikia nchini Morocco, Huku klabu hiyo ikishiriki kama mabingwa watetezi kutoka barani ulaya timu hiyo itamkosa staa wake Karim Benzema kwenye michuano hiyo.

