Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amethibisha kua klabu hiyo haitakata rufaa kupinga kadi nyekundu aliyopewa kiungo wake Carlos Casemiro aliyopewa wikiendi iliyomalizika dhidi Crystal Palace.
Kiungo Casemiro alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa ligi kuu ya Ungereza dhidi ya klabu ya Crystal Palace uliopigwa katika dimba la Old Trafford na kumfanya kiungo huyo kukosekana katika michezo mitatu inayofuta ya Manchester United.
Kocha Ten Hag wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kuelekea mchezo wao utakaopigw akesho katika dimba la Old Trafford dhidi ya klabu ya Leeds United ametanabaisha kua klabu hiyo haina mpango wakukata rufaa juu ya kadi ya kiungo wao.
Klabu ya Man United ilitazamiwa kukata rufaa juu ya kadi hiyo lakini kocha Erik Ten Hag amekanusha kuhusiana na suala hilo, Inaelezwa moja ya sababu iliyofanya klabu hiyo isikate rufaa ni kuhofia kukatilwa kwa rufaa halafu kiungo huyo akaongezewa mchezo mmoja na kufanya kukosa michezo minne badala ya mitatu kama awali.
Klabu ya Manchester United itamenyana na klabu ya Leeds United kesho jumatano katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza ambapo Man United itakua nyumbani, Mchezo huu utakua mchezo wa kwanza kwa kiungo Casemiro kuanza kuitumikia adhabu yake.

