Valverde: Nitarudi kwenye Ubora Wangu

Kiungo wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Uruguay Federico Valverde ameahidi kurudi kwenye ubora wake ambao alikua nao kabla ya michuano ya kombe la dunia.

Kiungo Federico Valverde alikua kwenye kiwango bora sana kabla ya michuano ya kombe la dunia ndani ya klabu yake ya Real Madrid mpaka kufikia kua moja ya wafungaji bora ndani ya kikosi hicho, Lakini ghafla anaonekana kuporomoka ghafla kutoka kwenye ubora wake.ValverdeKiungo huyo alikua moja ya wachezaji muhimu sana ndani ya kikosi cha kocha cha Carlo Ancelotti tangu msimu uliomalizika, Lakini ubora ulionekana kupanda mara dufu ndani ya msimu huu lakini baada ya michuano ya kombe la dunia kumalizika kiungo huyo anaonekana kushuka kiwango.

Kiungo Federico Valverde amekiri anatambua kua kabla ya michuano ya kombe la dunia alikua kwenye ubora mkubwa sana, Lakini ameahidi kidogokidogo atarudi kwenye ubora wake ambao alikua naop siku za karibuni haswa kabla ya michuano ya kombe la dunia.ValverdeKiungo huyo pia amegusia suala la mchezaji mwenzake ndani ya klabu hiyo Vinicius anapokutana na matatizo mbele ya wapinzani wake mara kwa mara, Huku akisema inabidi wamuache Vinicius afurahie npira wake kwa namna atakavyo.

Acha ujumbe