Klabu ya Liverpool ipo kwenye mazungumzo ya mkataba mpya na mshambuliaji wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Brazil Roberto Firmino,Mshambuliaji huyo ataongezewa mkataba mpya ndani ya klabu hiyo ukiwa wa muda mfupi.
Klabu ya Liverpool imefika sehemu nzuri kwenye mazungumzo na mshambuliaji wake Roberto Firmino kwajili ya kumpa mkataba mpya ambao unaelezwa utakua wa muda mfupi, Lakini mshambuliaji huyo amekubali kusaini mkataba wa kusalia Anfield.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp inaelezwa ndio sababu kubwa ya mshambuliaji huyo kupewa mkataba mpya wa kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo, Mshambuliaji huyo kwasasa amekua akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara ndani ya klabu hiyo.
Mshambuliaji Roberto Firmino amekua hapati nafasi ya kuanza mara kwa mara kwenye kikosi cha Liverpool na hiyo inatokana na majeraha ambayo yamekua yakimuandama mchezaji huyo, Lakini mshambuliaji huyo ameamua kusalia kwenye viunga vya Anfield.
Wakala wa mchezaji Roberto Firmino amethibitisha kua klabu hiyo na mteja wake wako kwenye sehemu nzuri ya katika mazungumzo ya kuongeza mkata mpya, Hivo mshambuliaji huyo yupo kwenye hatua za nzuri za kuendelea kusalia Anfield.

