Klabu ya Simba baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Horoya, wanatarajia kurejea hii leo nchini kwaajili ya kujiandaa na mchezo wa pili unaofuata ambao watakuwa wenyeji wa Raja Casablanca.

Lakini kabla ya kuanza safari ya kurejea watafanya mazoezi ndipo waanze kuja huku wakiwa na kazi kubwa ya kufanya dhidi ya Raja ambao wao ndio wanaongoza kundi C kwa kuifunga Vipers mabao 5.
Ikumbukwe kuwa Raja wana timu nzuri ambayo msimu juzi wa 2021 baada ya kuondolewa kwenye michuano ya Klabu Bingwa na kwenda kushiriki Kombe la Shirikisho walibeba ubingwa huo.
Hivyo itakuwa si rahisi kwa kocha Roberto kutojiandaa mapema na kujua jinsi ya kukabiliana na timu hiyo huku Simba wakiw ana kauli ya ” Kwa Mkapa Hatoki mtu”. Lakini je na safari hii hatoki mtu kweli?

Vilevile baada ya mwalimu kumkosa Saido Ntibanzokiza aliyesajiliwa dirisha dogo huku akiongeza kasi ya ufungaji kwa Wekundu wa Msimbazi anaweza kucheza mechi hiyo kama akiwa yupo fiti.
Mechi hiyo itapigwa Jumapili ya tarehe 18 majira ya saa 1:00 usiku huku Mnyama akihitaji ushindi ili ajiweke kwenye nafasi nzuri.

