Kiungo wa Simba Sadio Kanoute ataikosa Raja Casablanca baada ya kuonyeshwa kadi ya njano hapo jana baada ya kumchezea madhambi mchezaji wa Horoya.

Ikumbukwe pia Sadio alipewa kadi ya njano kwenye mechi dhidi ya Primeiro De Agosto ambayo waliitoa, hivyo kutokana na kupewa kadi mbili za njano mfululizo mechi ijayo dhidi ya Raja ataikosa.
Kiungo huyo licha ya kuwa na kazi nzuri anaifanya pale katikati, ndiye anayeongoza kwa kupewa kadi nyingi za njano katika ligi kuu ya NBC huku tayari mpaka sasa akiwa na jumla ya kadi za njano 9.
Kocha Mbrazil Roberto inabidi achague mchezaji mwingine wa kwenda kuziba nafasi ya Kanoute kwenye mchezo ujao kwani siku ni chache zimebaki na ana wachezaji wengi ambao wanacheza eneo hilo.

Mchezo huo kati ya Simba na Raja Casablanca ya nchini Morocco utapigwa tarehe 18 siku ya Jumapili majira ya saa 1:00 usiku

