Bellingham Ampongeza Adeyemi

Kiungo wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Uingereza Jude Bellingham amempongeza mcheza mwenzake wa klabu hiyo Karim Adeyemi baada ya kiwango alichokionesha dhidi ya klabu ya Chelsea.

Bellingham alivutiwa na mchezaji mwenzake Karim Adeyemi baada ya kufunga bao pekee ka ushindi katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya klabu ya Chelsea, Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani aliweza kufunga bao la uwezo binafsi katika mchezo huo.BellinghamKlabu ya Borussia Dortmund jana ilifanikiwa kuifunga klabu ya Chelsea katika mchezo wa hatua ya 16 bora ligi ya mabingwa ulaya katika dimba la Signal Iduna Park, Hivo kuwapa faida kuelekea mchezo wa marudiano jijini London utakaopigwa wiki mbili mbele.

Kiungo Bellingham licha kumsifu mchezaji mwenzake lakini pia alizungumzia mchezo huo ambao walifanikiwa kupata ushindi akisema walifanikiwa kucheza vizuri kipindi cha kwanza, Lakini Chelsea pia wakitengeneza nafasi lakini kipindi cha pili waliweza kutumia nafasi ambayo wamepata na kushinda mchezo.BellinghamKlabu ya Chelsea baada ya kupoteza mchezo wa jana imeendelea kua na mfululizo wa kutopata matokeo katika michezo yake ya hivi karibuni kwenye michuano yote, Jambo ambalo linamueka kwenye wakati mgumu zaidi kocha wa timu hiyo Graham Potter.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.