Henry Yuko Tayari Kuifundisha Marekani

Gwiji wa zamani wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Thiery Henry amesema yuko tayari kuchukua kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Marekani kama atapewa nafasi kama inavyosemekana.

Marekani wapo kwenye mkakati wa kutafuta kocha mpya wa kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya aliyekua kocha wa timu hiyo Gregg Berlahalter kumalizika mwishoni mwa mwaka jana, Taarifa zinaeleza kua gwiji Henry yupo kwenye orodha ya makocha ambao wanatajwa kupewa nafasi ya kua kocha wa timu ya taifa ya Marekani.HenryThiery Henry kwasasa amekua na uzoefu baada ya kuu kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji vipindi viwili vya michuano ya kombe la dunia akianzia Urusi mwaka 2018, na Qatar mwaka 2018 hivo gwiji huyo yupo tayari kuchukua timu yeyote na kuiongoza kama kocha mkuu.

Marekani ambaye imepata nafasi ya kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2026 hivo inataka kujiandaa mapema na kutengeneza timu bora ambayo italeta ushindani kwenye michuano hiyo, Hivo wanahitaji kocha ambaye ataweza kuwafikisha kwenye nchi ya ahadi.HenryGwiji Henry ambaye tayari ameshafundisha klabu moja na kua msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji kwa muda mrefu, Gwiji huyo ameonesha utayari wake pale alipoulizwa kuhusu kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Marekani ambayo inatafuta kocha kwasasa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.