Manchester City Yakabwa Koo Yalazimishwa Sare

Klabu ya Manchester City yakabwa koo ni baada ya imelazimishwa sare na klabu ya Nottingham Forest katika mchezo wa ligi kuu ya kuu ya Uingereza katika mchezo uliopigw akatika dimba la City Ground.

Klabu ya Manchester City ambayo katikati ya wiki ilifanikiwa kuwafunga vinara wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Arsenal kwa mabao matatu kwa moja, Lakini leo wamekutana na kizingiti baada ya klabu ya Nottingham Forest kuwalazimisha sare ya bao moja kwa moja.Manchester CityMabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Uingereza walifanikiwa kuutawala mpira kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo na kutengeneza nafasi kadhaa, Dakika ya 41 ya mchezo mchezaji Bernardo Silva alipiga shuti kali lililoipa bao la uongozi klabu hiyo na mpaka kwenda mapumziko walikua na uongozi wa bao moja kwa bila.

Manchester City walirejea kipindi cha pili wakiendelea kutafuta mabao zaidi wakijaribu kutengeneza nafasi ambazo hazikuzaa mabao mpaka pale dakika ya 84 Chris Wood akiipatia bao la kusawazisha klabu ya Nottingham Forest na mpaka mpira unamalizika matokeo yalikua bao moja kwa moja.Manchester CityKlabu ya Manchester City baada ya kutoka sare katika mchezo wa leo na kudondosha alama mbili katika mchezo huo, Sasa wamefikisha jumla ya alama 52 wakiwa nyuma ya vinara klabu ya Arsenal kwa tofauti ya alama mbili kwani Arsenal wao wameshinda mchezo wao dhidi ya Aston Villa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.