Ten Hag: Bruno Atabaki kua Nahodha

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesema kua kiungo wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Ureno Bruno Fernandes ataendelea kusalia kama nahodha wa klabu hiyo licha ya maneno yanayoendelea.

Taarifa zimeenea siku za karibuni kua kiungo huyo anaweza kuondolewa kua nahodha msaidi ndani ya klabu ya Manchester United, Lakini kocha Ten Hag ameweka wazi kua kiungo huyo ataendelea kua nahodha wa timu hiyo na hayo ambayo yanaendelea hayana nguvu ndani ya timu hiyo.Ten HagKocha huyo wakati anazungumza na wanahabari kuelekea mchezo wao wa Europa league dhidi ya Real Betis  na kusema ana furaha na kiungo huyo kuendelea kua nahodha wa klabu hiyo kwa kushirikiana na Harry Maguire na kusema kiungo huyo anafanya kazi kubwa ndani ya timu hiyo.

Kocha Ten Hag ameonesha kuvutiwa na kiwango ambacho anakionesha Bruno Fernandes ndani ya msimu huu, kwani mchezaji huyo amekua akijitoa kwa kiwango kikubwa kwajili ya kuisaidia klabu hiyo hivo kocha huyo anaona kiungo huyo anafaa kuendelea kua kiongozi kwenye timu hiyo.Ten HagBruno Fernandes ameibua maneno kwa mashabiki wa klabu hiyo siku za hivi karibuni baadhi yao wakitaka avuliwe unahodha ndani ya timu hiyo, Lakini kutokana na uimara wake ndani ya timu hiyo kocha Ten Hag anaona kiungo huyo bado anaendelea kua kiongozi ndani ya timu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.