Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag ameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tena tuzo ya kocha bora wa mwezi ndani ya ligi kuu ya Uingereza ndani ya mwezi Febuari.

Kocha Ten Hag ambaye alishafanikiwa kubeba tuzo hiyo baada ya kufanya vizuri ndani ya mwezi Septemba mwaka jana, Amefanikiwa kuingia kwenye kinyang’nyiro hicho ndani ya mwezi wa Febuari akiwa na makocha wengine wawili ambao ni Marco Silva wa Fulham pamoja na Antonio Conte wa Tottenham Hotspurs.ten hagKocha Ten Hag amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya mwezi Febuari kwani amefanikiwa kuiongoza klabu ya Manchester United kwenye michezo minne, Huku akifanikiwa kushinda michezo mitatu kati ya minne na kusuluhu mchezo mmoja.

Makocha wengine ambao wanawania tuzo hiyo Marco Silva wa Fulham ambaye kaiongoza timu hiyo kwenye michezo minne na kufanikiwa kushinda miwili na kusluhu miwili, Huku Antonio Conte akioongoza Tottenham michezo minne na kushinda mitatu na kufungwa mchezo mmoja.ten hagTuzo hizo zinatarajiwa kutolewa mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kupigiwa kura na mashabiki, Lakini mpaka sasa kocha wa Manchester United anaonekana kuongoza kinyang’anyiro hicho kwani kati ya makocha wote wanaoshindana kocha huyo ndio anaongoza kwa alama nyingi.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa