Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amewapongeza wachezzaji wake baada ya matokeo dhidi ya klabu ya West Ham jana baada ya kutangulia kufungwa na kusawazisha na baadae kupata matokeo ya ushindi.
Klabu ya Manchester United ilifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la Fa baada ya kufanikiwa kutoka nyuma kwa bao moja na kufunga mabao matatu, Jambo limemfanya kocha wa klabu hiyo kufurahishwa na wachezaji wake kwa kutokupaniki baada ya kufungwa na kutulia na mwisho kupata matokeo ya ushindi.Klabu ya Manchester United jana wakiwa kwenye dimba lao la Old Trafford walifanikiwa kushinda mabao matatu kwa moja na hapo ni baada ya kutanguliwa kwa bao moja lilifungwa na Said Benrahma, Huku Beki Norgard akijifunga kabla ya Alejandro Garnacho na Fred kufunga na kuiwezesha klabu hiyo kushinda mabao matatu.
Kocha Ten Hag alimpongeza kinda wa klabu hiyo Alejandro Garnacho baada ya kua na mchezo mzuri hapo jana baada ya kufunga bao la pili dakika ya 91 ya mchezo, Huku akiibuka kama mchezaji bora wa mchezo huo kutokana na ubora aliouonesha katika mchezo huo.Klabu ya Manchester United itasafiri hadi jijini Liverpool wikiendi hii kumenyana na klabu hiyo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza, Huku Man United wakiwa kwenye ubora mkubwa na Liverpool wao wakiwa wanataka kurudisha ubora wao mchezo huo untarajiwa kua mgumu kwa vilabu vyote viwili.