Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool kwasasa anakipiga ndani ya klabu Bayern Munich Sadio Mane anasema anaamini kua klabu yake ya zamani ya Liverpool itarejea kwenye ubora wake.

Klabu ya Liverpool imekua ikipitia kipindi kigumu tangu nyota Sadio Mane alipotimka klabuni hapo majira ya joto yaliyopita, Lakini staa huyo anaiona timu yake hiyo ya zamani inaweza kurudi kwenye ubora wake ambao imekua nao kwa misimu kadhaa iliymalizika.ManeKlabu ya Liverpool msimu huu inaonekana kua kwenye wakati mgumu sana kwani mpaka sasa inaonekana kuwania kushiriki ligi ya mabingwa ulaya, Kwani mpaka wakati huu klabu hiyo haionekani kuwania taji lolote ndani ya msimu huu.

Mchezaji Mane anasema kua Liverpool itarejea kwenye ubora wake kwani anaamini kwa kipindi cha hivi karibuni majeraha yamekua yakiiandama klabu hiyo na ndio sababu ya kufanya vizuri, Lakini vilevile pia anaamini kocha Klopp ataiongoza klabu hiyo kwenye mafanikio tena.ManeMshambuliaji Sadio Mane pia alizungumzia suala lake la kujiunga na klabu ya Bayern Munich akieleza kua alikutana na Ronaldo kwenye moja ya mgahawa nchini kwenye jiji la Mallorca, Huku akisema kua nyota huyo alimpongeza na kumueleza kua ni hatua nzuri yeye kujiunga na Bayern Munich.

 JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa