Beki mahiri wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi Virgil Van Dijk amesema ushindi wao dhidi ya Wolves jana unatoa taswira nzuri kuelekea mchezo wao dhidi ya Man United, Lakini pia akihitaji mashabiki wengi kujitokeza katika mchezo huo.
Klabu ya Liverpool watawakaribisha Manchester United katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza utaopigwa katika dimba la Anfield siku ya jumapili, Hivo Van Dijk anahitaji sana mashabiki wao wajae ili kuweza kuwapa hamasa kuelekea mchezo huo muhimu kwao.Klabu ya Liverpool wamekua hawako kwenye kiwango kizuri kwasasa kutoka na kudondosha alama mara kwa mara katika michezo yao tofauti tofauti, Lakini jana waliweza kupata ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya klabu ya Wolves kitu kinachoweza kuwapa nguvu kuelekea mchezo wao wa jumapili.
Van Dijk amesema wameweza kuchukua alama muhimu dhidi ya klabu ya Wolves japo walikua wapinzani wagumu kwao, Lakini amesema klabu ya Manchester ambayo wanakwenda kucheza nayo jumapili ni timu ambayo ipo kwenye ubora mkubwa kwasasa hivo wanajua mchezo utakua mgumu na ndio maana wanahitaji msaada wa mashbiki wao.Kocha Jurgen Klopp pia amezungumza na kuipongeza timu yake baada ya kupata matokeo dhidi ya klabu ya Wolves katika mchezo wao uliopigwa katika dimba la Anfield, Lakini aliwazungumzia Man United na kusema ni timu iliyopo kwenye kiwango bora kwasasa hivo anatarajia mchezo mgumu dhidi yao.