Rashford: Napenda Kucheza na Bruno Fernandes

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uingereza Marcus Rashford ameweka wazi na kusema kua anafurahishwa kucheza na kiungo wa klabu hiyo Bruno Fernandes.

Marcus Rashford amesema yeye anafurahia kucheza na kiungo Bruno Fernandes na kusema anampa sapoti kiungo huyo kwa asilimia mia moja, Kwani mshambuliaji huyo anasema kiungo anawafanya wachezaji wengine kwenye timu hyo kua viongozi wazuri .rashfordSiku za karibuni baada ya kichapo cha mabao saba kwa bila dhidi ya Liverpool na kiungo Bruno Fernandes amekua akiandamwa kutokana na kiwango ambacho alichokionesha katika mchezo huo, Hivo kupelekea mashabiki wengi kumnyooshea kidole na kusema avuliwe kitambaa cha unahodha klabuni hapo.

Mshambuliaji Marcus Rashford amesema yeye yuko nyuma ya nahodha wake huyo msaidizi ndani ya klabu hiyo, Kauli ya mshambuliaji huyo inaonesha wazi anapuuzia maneno yanayoendelea kwa miongoni mwa mashabiki wa Manchester United ambao wanamshambulia kiungo huyo.rashfordKiungo Bruno Fernandes amekua moja ya wachezaji wenye mchango mkubwa sana ndani ya klabu ya Manchester United tangu ajiunge klabuni hapo mwaka 2020, Kiungo huyo amekua akijitoa kwa kiwango kikubwa ndani ya timu hiyo na ndio sababu amekua akikubalika na wachezaji wenzake pia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.