Rashford: Amshukuru Ten Hag

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Marcus Rashford ambaye amekua na kiwango bora sana kwasasa amemshukuru kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag kwa namna alivyomsaidia kua vizuri.

Marcus Rashford anasema kocha wa klabu hiyo kwasasa Erik Ten Hag ametengeneza mazingira mazuri ya kufanya kile ambacho klabu hiyo inafanya kwasasa akiwemo yeye pamoja wachezaji wote kwa ujumla, Kocha huyo amefanikiw akwa kiwango kikubwa kuijenga timu hiyo kwa kipindi kifupi na kuonekana tishio kwasasa.RashfordMshambuliaji huyo anasema kutokana na mazingira ambayo kocha huyo ameyatengeneza ndani ya timu hiyo na kufanikiw akufanya vizuri kwasasa, Basi yeye binafsi anaamini wataendelea kufanya vizuri kama wataendelea kushinda michezo yao.

Marcus Rashford alikua na msimu mbaya sana mwaka 2021/22 akifunga mabao matano kwenye michuano yote, Lakini msimu huu chini ya kocha Erik Ten Hag ameamka na kufanya vizuri sana akiwa ameshapachika mabao 24 kwenye michuano yote msimu huu mpaka sasa.RashfordKocha Ten Hag amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuijenga timu hiyo kwa kipindi kifupi, Huku wengine wakienda mbali na kuona sasa kama kocha huyo ndio mrithi sahihi wa kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United ambaye ameipa mafanikio makubwa timu hiyo Sir Alex Ferguson.

Acha ujumbe