Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesema uchambuzi unaofanywa na malijendi wa zamani wa klabu hiyo kwenye vitu mbalimbali vya habari unaathiri wachezaji wake.

Kuna wachezaji mbalimbali wa zamani wa klabu hiyo kwasasa wanafanya kazi kwenye vyombo vya habari kama Roy Keane, Rio Ferdinand, Paul Scholes, pamoja na Gary Neville ambao mara nyingi wamekua wakikosoa wachezaji wa klabu hiyo jambo ambalo kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag hafurahishwi nalo.Ten hagMagwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United mara nyingi wamekua wakikosoa wachezaji wa klabu hiyo pale ambapo wanafanya vibaya na kila siku wamekua wakitafuta udhaifu jambo ambalo kocha huyo wa raia wa kimataifa wa Uholanzi anaona sio sawa na linawaathiri wachezaji wake.

Kocha Erik Ten Hag ambaye amejizoelea sifa kedekede siku za karibuni kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha ndani ya klabu hiyo, Leo kocha huyo ataiongoza klabu ya Manchester United kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Carabao dhidi ya Newcastle United.Ten hagKocha Ten Hag licha ya kutokufurahishwa na kitendo cha wachezaji wake kukosolewa mara kwa mara na magwiji wa klabu hiyo, Lakini kocha huyo anasema anajaribu kuwaelewa magwiji hao kwani wanakosoa sana kwasababu ni klabu ambayo wanaipenda sana na wanatamani ifanye vizuri.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa