Pioli Aionya Milan Kutokukaa Nyuma Dhidi ya Spurs

Kocha wa klabu ya soka ya Ac Milan Stefano Pioli amewaonya wachezaji wake kuelekea mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya Tottenham na kuwataka kutozuia mda wote.

Klabu ya Ac Milan itacheza dhidi ya klabu ya Tottenham ambayo watakua nyumbani huku klabu ya Ac Milan wakiwa na faida ya goli moja ambalo walishinda wakiwa nyumbani katika dimba la San Siro, Hivo kocha Pioli amewakumbusha wachezaji wake kutobweteka katika mchezo huo.pioliKlabu ya Ac Milan imekua ikitaka kurudi kwenye ubora wake ndani ya ligi ya mabingwa barani ulaya kwa kipindi kirefu kidogo imekua kwenye kipindi cha mpito, Lakini misimu miwili nyuma imeonekana kuanza kushiriki michuano ya ulaya na dhamira yake ya kutaka kufanya vizuri.

Kocha Pioli wakati akifanya mazungumzo na wanahabari na kusema anatambua kua mchezo wa leo utakua mgumu kwao na wanajua wapinzani wao watashambulia kwa kasi, Lakini wao hawatakaa nyuma kwani faida yao ni ndogo watajitahidi kushambulia katika mchezo huo.pioliKocha Pioli anasema wamejiandaa katika mchezo huo dhidi ya Tottenham Hotspurs lakini kocha huyo anaamini vijana wake wako tayari kukabiliana na changamoto watakayokutana nayo mbele yao, Kwani anatambua watakutana na mpinzani ambaye ameandaliwa kwelikweli.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.