Henderson Awaonya Wenzake ndani ya Liverpool

Nahodha wa klabu ya Liverpool Jordan Henderson amewaonya wachezaji wenzaji wasijiamini kupitiliza baada ya kufanikiwa kuifunga klabu ya Manchester United kwa mabao 7-0 katika mchezo wa ligi ku ya Uingereza wikiendi iliyomalizika.

Klabu ya Liverpool iliweza kuishusia klabu ya Manchester United kipigo cha kihistoria siku ya jumapili baada ya kuifunga klabu hiyo kwa mabao 7-0 mchezo uliopigwa katika dimba la Anfield, Lakini Henderson anaona ushindi huo hautakiwa kuwafanya wajiamini sana kuelekea michezo mingine.HendersonLiverpool wamekua hawana msimu mzuri japo walifanikiwa kuifunga Man United kipigo cha aibu wikiendi iliyomalizika, Ikiwa mpaka sasa klabu hiyo iko nyuma kwa alama saba dhidi ya klabu ya Manchester United ambayo inakamata nafasi ya tatu Liverpool wakiwa nafasi ya tatu.

Jordan Henderson katika mazungumzo na tovoti ya klabu hiyo alisema “Naamini tunaweza kutumia ushindi katika njia nzuri, ila hatutakiwi kujiamini zaidi baada ya kupata matokeo haya,  Tutakutana na vipimo tofauti tofauti kuanzia sasa mpaka msimu unamalizika na unapaswa kubaki chanya, tunatakiwa kua tayari, na njaa kama tulivyo sasa, Hiyo itatupatia nafasi nzuri ya kumaliza mziki vizuri”HendersonKlabu ya Liverpool itakua na mtihani wa kuendeleza kile ambacho wamekifanya dhidi ya Man United katika michezo yao ijayo, Kitu ambacho nahodha Henderson amesema kua wanatakiwa kua sawa na njaa ya kuendelea kupambana kama ambavyo wanaonesha njaa hiyo kwasasasa lakini wasijiamini kupita kiasi kwani inaweza kuwagharimu.

Acha ujumbe